Nywele hukua tofauti kwa kila mtu, wengine zinakua haraka sana wengine taratibu kama kinyonga.
Sababu kuu tatu zinazosaidia ukuaji wa nywele ni
1.usafi
2.kuziacha nywele zipumue, mitindo michache isiyovuta sana nk.
3.kama ilivyo kwa bustani nzuri, upaliliaji!
USAFI
je waosha nywele zako mara ngapi kwa mwezi, wiki, siku? waosha kwa kutumia nini?
mimi huosha mara moja kwa wiki,
kipindi nywele zangu zilikua fupi nilikua nikiosha tu bila wasiwasi ila sasa zimekuwa ndefu na zinashikamana sana hivyo basi inanibidi kuosha kwa mafungu mafungu hii inapunguza ushikamanaji wa nywele na pia ukatikaji wa nywele.
usafi wa mwili na roho je?
kula vyakula vyenye virutubisho, samaki na karanga hukuza nywele,kunywa maji mengi ondoa stress, kuwa mwenye furaha .
MISUKO
Kuna misuko jamani mpaka unameza panadol, je wahisi kitabaki kitu kweli?
suka style tulivu, style zenye upendo na ngozi yako. ukiona msusi anataka kukutoa roho achana naye tafuta mwenye mkono mlaini .
pia usiziache wazi sana penda kuzifunika wakati wa kulala, funga kiremba huko hupunguza makali ya mto kugusana na nywele na kukatika kwa nywele.
MBOLEA
je wewe watumia mbolea gani na unaitumiaje?
wanasayansi wamezibitisha njia kuu tatu ambazo husaidia kurutubisha mizizi na nywele pia kubaki katika hali ya mng'aro wa kuvutia.
moisture (maji) nyunyizia tumaji kidogo kuanzia chini kwenda juu, usiloweshe nywele fanya tu kuwe na unyevunyevu. kishua paka mafuta mepesi kama alizeti au ya nazi kishua paka mgando kama shea butter au cream za nywele. funga mabutu lala. waweza fanya hivi mara mbili hadi tatu kwa wiki kama nywele zako ni ngumu sana.
Harrah's Philadelphia Casino & Racetrack - JT Hub
ReplyDeleteInformation 경상남도 출장마사지 and 익산 출장안마 reviews for Harrah's Philadelphia Casino 김해 출장샵 & Racetrack in Chester, PA. Discover locations, hours, directions, 수원 출장안마 and 인천광역 출장안마 information for Harrah's