Translate

Thursday, 12 February 2015

Thursday, 29 January 2015

Ukuzaji wa nywele

Nywele hukua tofauti kwa kila mtu, wengine zinakua haraka sana wengine taratibu kama kinyonga.
Sababu kuu tatu zinazosaidia ukuaji wa nywele ni
1.usafi
2.kuziacha nywele zipumue, mitindo michache isiyovuta sana nk.
3.kama ilivyo kwa bustani nzuri, upaliliaji!

USAFI
je waosha nywele zako mara ngapi kwa mwezi, wiki, siku?  waosha kwa kutumia nini?
mimi huosha mara moja kwa wiki,
kipindi nywele zangu zilikua fupi nilikua nikiosha tu bila wasiwasi ila sasa zimekuwa ndefu na zinashikamana sana hivyo basi inanibidi kuosha kwa mafungu mafungu hii inapunguza ushikamanaji wa nywele na pia ukatikaji wa nywele.
usafi wa mwili na roho je?
kula vyakula vyenye virutubisho, samaki na karanga hukuza nywele,kunywa maji mengi ondoa stress, kuwa mwenye furaha .

MISUKO
Kuna misuko jamani mpaka unameza panadol, je wahisi kitabaki kitu kweli?
suka style tulivu, style zenye upendo na ngozi yako. ukiona msusi anataka kukutoa roho achana naye tafuta mwenye mkono mlaini .
pia usiziache wazi sana penda kuzifunika wakati wa kulala, funga kiremba huko hupunguza makali ya mto kugusana na nywele na kukatika kwa nywele.

MBOLEA
je wewe watumia mbolea gani na unaitumiaje?
wanasayansi wamezibitisha njia kuu tatu ambazo husaidia kurutubisha mizizi na nywele pia kubaki katika hali ya mng'aro wa kuvutia.
moisture (maji) nyunyizia tumaji kidogo kuanzia chini kwenda juu, usiloweshe nywele fanya tu kuwe na unyevunyevu. kishua paka mafuta mepesi kama alizeti au ya nazi kishua paka mgando kama shea butter au cream za nywele. funga mabutu lala. waweza fanya hivi mara mbili hadi tatu kwa wiki kama nywele zako ni ngumu sana.

nywele fupi

matunzo yake ni marahisi zaidi, osha paka conditioner paka mafuta chana

style mbali mbali

kuanzia nilikotoka mpaka leo hii

faida za castor oil

mafuta haya yamedhibitisha ukuzaji nywele haraka kwa muda mrefu sasa,
ukinunua yale ya kariakoo ni mazito na yananata kama asali njia rahisi ni kuyachanganya na mafuta mengine au maji ya mawaridi pia yanapatikana kariakoo.
Mafuta haya huchangamsha mfumo wa damu na kufungua njia ya mizizi ya nywele hivyo kuchochea ukuaji wa nywele.

karibu

mafuta asilia yanayosaidia kukuza nywele ni kitunguu swaumu (garlic oil) alizeti (olive oil) nazi (Coconut oil) nyonyo (castor oil) vitamin A oil and vitamin E oil, mafuta ya alizeti (sunflower oil), lavender oil, teatree oil,

sio lazima utumie yote haya unaweza changanya mawili matatu kwa kikopo chako unanyunyizia au sugulia kwa ngozi, fanya massage ya kichwa kwa dakika kumi na tano yatosha kila siku.. kama nywele zako kavu kama zina mafuta basi fanya mara moja au mbili kwa wiki.